KAULI ZA WABUNGE UPINZANI JUU YA BAJETI

Akizungumza baada ya Waziri wa Fedha na Mipango kuwasilisha mapendekezo ya ukomo wa bajeti hiyo pamoja na mpango wa maendeleo kwa mwaka huo, Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, ambaye pia ni Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe (Chadema), alisema mambo mema yamefanywa.