Chuo Kikuu cha Kiislamu nchini Misri, kimelaani vikali jinai ya kibaguzi na chuki dhidi ya dini ya Uislamu iliyofanywa na mtu mmoja mwenye misimamo ya kufurutu ada mjini Brussels, Ubelgiji dhidi ya mwanamke mmoja aliyekuwa amevaa vazi la staha la hijabu nchini humo.

Taarifa iliyotolewa na al-Azhar imesema kuwa, jinai hiyo mbaya kabisa ya kumkanyaga bila huruma mwanamke wa Kiislamu inayotokana na chuki na ubaguzi, haina tofauti yoyote na jinai zinazofanywa na wanachama wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh na al-Qaidah katika maeneo tofauti ya dunia. Taarifa hiyo imeongeza kuwa, mauaji dhidi ya mwanamke huyo wa Kiislamu aliyekuwa mlemavu wa viungo, yamesababishwa na matamshi ya chuki dhidi ya dini ya Kiislamu barani Ulaya. Imesema kuwa, makundi ya mrengo wa kulia na yenye kufurutu ada barani humo yamekuwa yakiyaunga mkono matamshi hayo ya kibaguzi huku kidhahiri yakijifanya kupinga mienendo hiyo ya kibaguzi. Kufuatia hali hiyo Chuo Kikuu cha Kiislamu cha al-Azhar nchini Misri kimeitaka serikali na asasi barani Ulaya, kupasisha azimio la kulaani matamshi ya ubaguzi na dhidi ya Uislamu barani humo kwa lengo la kuzuia vitendo kama hivyo. Aidha al-Azhar imeitaka serikali ya Brussels kuwachukulia hatua kali wahusika wa jinai hizo za kikatili. Inafaa kuashiria hapa kwamba, mtu mmoja mwenye misimamo ya kufurutu ada alimuua kwa kumkanyaga na gari mwanamke mmoja wa Kiislamu aliyekuwa amevalia hijabu katika eneo la Molenbeek, mjini Brussels Ubelgiji.

Related Posts

suscipit sunt necessitatibus
VPS by Dorian Grey

Comments (5)

Dorian Gray, 20:45, Feb. 28/2014

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit. Asperiores earum, doloribus at voluptates dolorem magnam, ducimus enim quibusdam accusantium deserunt dignissimos a impedit id ut. Cum aliquam distinctio fugiat sunt.

reply
Dorian Gray, 20:45, Feb. 28/2014

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit. Asperiores earum, doloribus at voluptates dolorem magnam, ducimus enim quibusdam accusantium

reply
Dorian Gray, 20:45, Feb. 28/2014

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit. Asperiores earum, doloribus at voluptates dolorem magnam, ducimus enim quibusdam accusantium deserunt dignissimos a impedit id ut. Cum aliquam distinctio fugiat sunt.

reply