Obama: Waislamu ni wahanga wa ugaidi
Rais Barack Obama wa Marekani amekiri kwamba Waislamu ni wahanga wa ugaidi.Obama ambaye alikuwa kihutubia katika shughuli za kidini mjini Washington amesisitiza kuwa Wakristo na Waislamu wamekuwa wahanga wa ugaidi na kwamba lengo la magaidi ni kudhoofisha imani za watu na kueneza chuki na mtazamo mbaya kuhusu dini na mbari tofauti.

Al Azhar yalaani mauaji dhidi ya mwanamke mva

Chuo Kikuu cha Kiislamu nchini Misri, kimelaani vikali jinai ya kibaguzi na chuki dhidi ya dini ya Uislamu iliyofanywa na mtu mmoja mwenye misimamo ya kufurutu ada mjini Brussels, Ubelgiji dhidi ya mwanamke mmoja aliyekuwa amevaa vazi la staha la hijabu nchini humo.

Viongozi wa Wakristo Senegal watunukiwa zawad

Mwakilishi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa (SAW) nchini Senegal amekutana na viongozi wa Wakristo nchini humo na kuwakabidhi zawadi ya nakala ya Qur’ani iliyotarjumiwa kwa lugha ya Kifaransa.

KAULI ZA WABUNGE UPINZANI JUU YA BAJETI

Akizungumza baada ya Waziri wa Fedha na Mipango kuwasilisha mapendekezo ya ukomo wa bajeti hiyo pamoja na mpango wa maendeleo kwa mwaka huo, Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, ambaye pia ni Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe (Chadema), alisema mambo mema yamefanywa.